Worldwide Swahili Meetup Message Board › CHANGAMOTO KWA WASEMAJI WA LUGHA YA KISWAHILI POPOTE PALE WALIPO

CHANGAMOTO KWA WASEMAJI WA LUGHA YA KISWAHILI POPOTE PALE WALIPO

A former member
Posted Jun 17, 2005 1:02 AM
Post #: 2
Huko tanzania Kiswahili kimeshamiri sana na siku hizi maneno mapya yanazuka kila siku. Je, kuna Mtanzania anayeweza kuorodhesha maneno hayo mapya pamoja na maana na matumizi ili siye tulioko nje tuyafahamu pia. Mathalan, utandawazi = globalization. Je, kuna mengine kama neno hili? Au kuna maneno ya mitaani pia? Yote ni sehemu ya lugha na wanalugha hatuna budi tuyajue na kuweza kuyatumia maneno hayo. Mushkeli uliopo ni kuwa magazeti ya Kiswahili si rahisi kuyapata huku wala kwenye uwanda!crying
Powered by mvnForum